Quantcast
Channel: JamiiForums | The Home of Great Thinkers - Sports
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5565

Uharibifu viti taifa: Simba waishangaa TFF kulipa faini !

$
0
0
BAADA ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kukubali kulipa sh.milioni 15 kutokana na uharibifu Uwanja wa Taifa uliofanywa na mashabiki wakati wa mechi ya Yanga na Al Alhy ya Misri walipocheza mechi yao ya Ligi ya Mabingwa, Simba wamepinga hatua hiyo ya TFF, anaripoti Mwandishi Wetu.
Katika mechi hiyo iliyochezwa Machi Mosi, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baadhi ya mashabiki wa soka waling'oa viti na hivyo Serikali ikawataka TFF kulipia gharama hizo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Simba Ezekiel Kamwaga alisema kuwa wao kama Simba wanapinga kitendo hicho cha TFF kulipa gharama hizo wakati mchezo huo ulikuwa ni baina ya Yanga na Al Ahly.
"Kanuni za CAF na FIFA zinasema kuwa timu mwenyeji anatakiwa kusimamia mchezo mzima likiwepo na suala la ulinzi na kama kutakuwa kuna tatizo lolote mwenyeji anatakiwa kuwajibika sasa leo iweje TFF, iseme inalipa fedha hizo badala ya Yanga?" Alihoji Kamwaga.
Alisema wao wakati wanacheza mchezo wa Ligi Kuu mzunguko wa kwanza na Kagera Sugar mashabiki waling'oa viti na TFF iliwalipisha sh.milioni 25 kwa vurugu hizo kwa kuwa wao ndiyo walikuwa wenyeji wa mchezo huo, lakini tatizo hilo limetokea kwa Yanga TFF, wanawalipia kama wameamua kuwalipia basi nao warudishiwe fedha zao walizokatwa.
Mashabiki wa Simba walifanya vurugu hizo katika mchezo huo baada ya Kagera Sugar kusawazisha bao la pili dakika za mwisho za mchezo huo wakidai kuwa mwamuzi wa mchezo huo alichezesha mchezo huo kwa zaidi ya dakika 90 baada ya zile za nyongeza kumalizika.
Alisema baada ya mchezo huo kesho yake TFF walichukua polisi na kuanza kutembelea kwenye matawi ya Simba na kuwakamata mashabiki wa timu hiyo na kuwafungulia kesi, lakini kwa Yanga hawakufanya hivyo.
"Baada ya mchezo huo kesho yake TFF, walikwenda tawi la Mpira Pesa, Ubungo Terminal na matawi mengine kuwakamata watu na wengine hawakuwepo kabisa uwanjani na kuwafungulia kesi mpaka sasa tunadaiwa milioni 21 polisi hatujalipa," alisema Kamwaga.
Aliongeza kuwa wao msimamo wao ni kutaka kulipwa fedha zao milioni 25 walizokuwa wanakatwa katika mapato ya mechi, kama TFF imeamua kulipa fedha hizo.



Majira.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 5565

Trending Articles