Quantcast
Channel: JamiiForums | The Home of Great Thinkers - Sports
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5565

Bodi ya Ligi na TFF ndani ya bifu zito

$
0
0
Taarifa za uhakika ambazo mtandao
huu umezipata ni kwamba kuna hali ya
kutoelewana kati ya TFF na bodi ya ligi. Chanzo cha kutokuwepo kwa
maelewano mazuri baina ya uongozi
wa bodi na TFF ni kutokana na viongozi
wa bodi ya ligi kukataa kukaguliwa
mahesabu ya matumizi yao ya fedha. Inasemekana kwamba uongozi wa
Jamal Malinzi ulivyoingia madarakani
uliwasaliana na bodi ya ligi ukiwaeleza
kwamba ungewatumia mkaguzi wa
mahesabu bodi ya ligi kwa ajili ya
kukagua matumizi yao. Lakini katika hali ya kushangaza bila
sababu ya msingi na yenye mashiko
uongozi wa bodi ya ligi ulikataa
kumpokea mkaguzi wa mahesabu, hali
iliyopelekea kutokuelewana baina ya
TFF na bodi hiyo.
Source: Shaffih Dauda

Viewing all articles
Browse latest Browse all 5565

Trending Articles