Quantcast
Channel: JamiiForums | The Home of Great Thinkers - Sports
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5565

News Alert: World top scorer: Ngasa awafunika messi na neymar

$
0
0
Click image for larger version. 

Name:	ngasa.jpg 
Views:	0 
Size:	88.4 KB 
ID:	158168

Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa amewapiku nyota wa Barcelona, Lionel Messi, Neymar kwa ufungaji wa mabao kwa mwaka 2014, huku akiachwa na kinara wa ufungaji Cristiano Ronaldo kwa magoli matatu tu. Katika orodha iliyochapishwa na mtandao IFFHS unaojihusisha na masuala ya takwimu za soka unamwonyesha Ngassa akiwa katika nafasi ya 4 katika orodha ya wafungaji 26 bora kwa mwaka huu akiwa amezifumania nyavu mara sita akiwa na kikosi cha Yanga.

Ngassa ameingia kwenye orodha hiyo baada ya kufunga mabao sita katika mechi ya awali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Komorozine ya Comoro. Pamoja na Yanga kuondolewa kwenye michuano hiyo na Al Ahly mwezi uliopita bado Ngassa anafungana na Haythem Jouini wa Esperance wakiwa vinara wa ufungaji wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Mwanasoka Bora wa Mwaka, Cristiano Ronaldo wa Ureno anashikilia usukani kwenye orodha hiyo ya ufungaji akiwa amefunga mabao tisa mwaka huu.
Mreno huyo alifunga mabao mawili dhidi ya Borussia Dortmund na mawili tena dhidi ya FC Bayern Munich na kuiongoza Real Madrid kufuzu kwa fainali ya Ligi ya Mabingwa UEFA. Ronaldo anafuatiwa kwa karibu na Mhispania Juan Belencoso anayecheza Kitchee SC ya Hong Kong ambaye ndiye mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Asia akiwa na mabao manane. Wachezaji waliofunga mabao saba kila mmoja ni Waafrika wawili (Mmorocco Mouhcine Iajour wa Raja AC Casablanca na nahodha wa Ghana, Asamoah Gyan anayechezeza Al Ain FC).
Pia Waasia wawili (raia wa Vietnam, Nguyen Van Quyet wa Ha Noi T&T F.C na Msyria Omar Al Soma wa Al-Qadsia). Vilevile yupo nyota mmoja wa Amerika Kusini (Mbrazili Paulo Rangel wa Selangor FA). Waliofunga mabao sita mwaka huu ni Ngassa (Yanga), Nasser Al-Shamrani (Al-Hilal FC), Kudakwashe Musharu (How Mine), Haythem Jouini (Esperance). Jumla ya wachezaji 26 wamefunga zaidi ya mabao matano, ila jambo la kushangaza Lionel Messi hayupo kati yao. Tangu mwaka 1991, IFFHS imekuwa ikipiga hesabu na kutoa orodha ya wafungaji bora wa mwaka wa dunia kwa kuangalia mabao wanayofunga kuanzia Januari hadi Desemba 31. Wafungaji hao wanapatikana kwa kuzingatia mabao waliyofunga kwenye michuano ya kufuzu kushiriki Fainali za Kombe la Dunia, michuano ya mabara kwa timu za taifa, Olimpiki, pamoja na mashindano ya klabu ya kimataifa

Listi nzima ya wafungaji bora wa dunia WORLD TOP SCORER
Attached Thumbnails
Click image for larger version. 

Name:	ngasa.jpg 
Views:	N/A 
Size:	88.4 KB 
ID:	158168  

Viewing all articles
Browse latest Browse all 5565

Trending Articles