Quantcast
Channel: JamiiForums | The Home of Great Thinkers - Sports
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5565

Nawaza Mbali....Siku Maximo atakapotimuliwa Jangwani na Yanga!!!

$
0
0
Maximo hatimaye amesaini mkataba mnono wa kuifundisha Yanga kwa miaka miwili. Hongera sana Maximo,
binafsi nakutambua vyema na una NIDHAMU kubwa sana ya mpira ambayo wachezaji wetu wengi hawana.

Tatizo la klabu zetu hizi kongwe Simba na Yanga wanataka matokeo mazuri na tena kwa muda mfupi, na wewe
una falsafa ya kujenga timu yenye nidhamu na vijana wadogo....Hapa ndipo naona kuna tatizo kubwa sana..
Hizi club zetu mpaka wazee nao wana nafasi, makomandoo, wafadhili wote hawa ni ngumu sana kuwafurahisha.

Binafsi nawaza sana siku ambayo utakuwa unafukuzwa hapo jangwani......sifa zako zote zitapotea. Na hizi club
mbili zina tabia ya KUZULUMU mishahara, mpaka uende TFF au FIFA, Maximo jiandae na mengi.

Maximo, usisahau kuja Dodoma!!!!

Mandla.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 5565

Trending Articles