Quantcast
Channel: JamiiForums | The Home of Great Thinkers - Sports
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5565

Kocha Mexime: Nimepandisha ‘CV’ kuifunga Yanga ya Maximo

$
0
0




KOCHA Mkuu wa timu ya Mtibwa Sugar ya Manungu, Morogoro, Mecky Mexime amewashukuru wachezaji wake kwa kuifunga Yanga na hivyo kumfanya apandishe wasifu (CV) wake mbele ya mwalimu wake mkuu katika soka.

Yanga kwa sasa inanolewa na Marcio Maximo, raia wa Brazil ambaye kwa miaka minne aliwahi kuifundisha timu ya Taifa, Taifa Stars wakati Mexime akiwa beki na nahodha wake.
Mexime alisema hayo baada ya kumalizika kwa mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga uliofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Jamhuri hapa ambao Mtibwa Sugar iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Hivyo alisema amefurahi kupata ushindi huo na zaidi ni kupata ushindi dhidi ya kocha wake mkuu wa zamani wa Taifa Stars, Maximo ambaye pia alimshauri asomee kazi ya ukocha.
“Napenda kuwashukuru wachezaji wangu kwa ushindi huu, sasa wameipandisha juu CV (wasifu) yangu kwani timu tulioifunga inafundishwa na kocha Maximo ambaye mimi nilikuwa ni mwanafunzi wake Taifa Stars,” alisema Mexime.

“Ushindi huu si wangu pekee, ni wa wachezaji na timu kwa ujumla kwa maana mimi ni kocha sichezi uwanjani, mchango wangu ni kuwafundisha na kutoa maelekezo ambayo yakitekelezwa kwa vitendo yanazaa matunda.”

Kwa mujibu wa kocha huyo, kabla ya kustaafu soka akiwa katika timu ya Taifa, Maximo ndiye aliyemshauri akiacha soka, ajifunze kazi ya ukocha na baada ya kustaafu, alitekeleza na sasa anainoa timu yake ya Mtibwa Sugar.

“Siku zote mashabiki wa soka wanapoona timu isiyokuwa na jina kubwa inapocheza na yenye jina kubwa haipewi nafasi ya kushinda kama ilivyo kwa mchezo huu wakiipa Yanga nafasi kubwa ya kushinda,” alisema Mexime.

Kocha huyo hakupenda kubashiri makubwa zaidi katika michezo inayofuata, akisema Ligi Kuu ndio imeanza na safari ni ndefu na ushindi huo pia umeleta hamasa kwa wachezaji, viongozi na wapenzi wa timu hiyo kuiona ikiendelea kufanya vizuri michezo ijayo.

CHANZO: Habari Leo

Viewing all articles
Browse latest Browse all 5565

Trending Articles