Quantcast
Channel: JamiiForums | The Home of Great Thinkers - Sports
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5565

FC Barcelona yapata 100

$
0
0
Baada ya ushindi wake wa jana dhidi ya Malaga wa4-1,Barcelona imeweka rekodi mpya La Liga kwa kujikusanyia alama 100 na na mabao 115 ya kufunga na hatimaye kutwaa ubingwa. Mabao ya David Villa,Cesc Fabregas,Martin Montoya na Andres Iniesta yalitosha kuipa ushindi Barcelona.

Bao la Malaga lilipachikwa na Pedro Morales. Huku Barcelona ikimaliza kinara kwa tofauti ya alama 15 dhidi ya mshindi wa pili Real Madrid,mshambuliaji Lionel Messi amekuwa mfungaji bora wa La Liga kwa kupachika mabao 46 ya ligi akifuatiwa na Christiano Ronaldo(34) na Falcao(28).

Wakati huo huo, timu nne zitakazoshiriki Klabu Bingwa Barani Ulaya msimu ujao zimepatikana toka La Liga kukiwa na mabadiliko makubwa.

Mwaka jana,timu zilizofuzu UCL zilikuwa ni Real Madrid,Barcelona,Valencia na Malaga. Mwaka huu ni Barcelona,Real Madrid,Atletico Madrid na Real Sociedad. Jana,Valencia walizabwa mabao 4-3 na Sevilla wakati Sociedad walipata ushindi muhimu wa 1-0 dhidi ya Derpotivo LaCoruna. Kipigo kwa Valencia kilizima ndoto zao za kucheza UCL.

Timu zilizoshuka daraja ni Derpotivo la Coruna,RealZaragoza na Mallorca.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 5565

Trending Articles