Vyombo kadhaa vya habari vimemripoti Naib Waziri wa Wizara inayoshughulikia michezo akikosoa uteuzi wa Kamati ya TFF ambayo huenda itahusika na kusikiliza rufaa ya Jamal Malinzi iwapo atagombea tena urais wa TFF baada ya Katiba mpya na iwapo atawekewa tena pingamizi na ikakubaliwa.
Hili linatokea wakati wadau wote wakiwa hawana kauli zozote dhidi ya uteuzi huo, hata kama kauli ya Bw. Makalla ina mantiki. Ingetegemewa kwamba kabla ya kutoa kauli hiyo iliyonukuliwa na vyombo vya habari, angekutana kwanza na pande husika (TFF, BMT na hata walioteuliwa na kuridhia) na kuyazungumza haya kiutu uzima. Labda kama kungetokea suitafaham (wengine huita sintofaham) baina yao, ndio angeweza kulirusha hewani.
Kama kuna swala la michezo, hasa mpira wa miguu, ambalo lingehitaji kauli ya Serikali zaidi kwa sasa, basi ni hili la mkataba wa kurusha matangazo anwai (live) ya Ligi Kuu ya Vodacom. Lakini kwa hilo amebaki kimya.
Hoja yangu ni kwamba : (1) Ni sahihi kwa Serikali kukalia kimya hili moja na ikalitolea kauli hili la pili? (2) hatupalii njia ya kurejea upya kwenye mgongano na FIFA kwa Serikali kuonekana inaingilia maswala ya TFF? (3) Kauli hii haileti shaka ya kuwapo uhusiano wa kimkakati (strategic relationship) baina ya Bw. Makalla na Bw. Jamal Malinzi? (4) Kwa nini ikaichukua Serikali muda mrefu kutoa kauli hiyo, baada ya Kamati yenyewe kuteuliwa? (5) Kwa nini Bw. Makalla aishupalie Kamati hiyo tu wakati TFF iliteua Kamati nyingine kadhaa? Hizo nyingine zinahalalika kwa katiba batili anayoisema Bw. Makalla?
Tanbihi (caution/disclaimer): Mtoa hoja ni mdau wa soka, lakini si shabiki wa upande wowote unaoweza kuwa na maslahi kwenye uchaguzi ujao wa TFF.