Quantcast
Channel: JamiiForums | The Home of Great Thinkers - Sports
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5565

Mtanzania bingwa kuruka kamba

$
0
0
Mtanzania aliyekulia katika mazingira magumu, Hamisi Kondo ametawazwa bingwa wa mchezo wa kuruka kamba duniani.
Kondo ambaye ni yatima, amewasili nchini Tanzania kutoka Marekani alikoshiriki mchezo huo, na kupongezwa na watu wa kada mbalimbali, wakamsifu kwa kuipeperusha vyema bendera ya taifa.
Kifuta machozi hicho kimekuja siku chache tu baada ya timu ya soka Tanzania kutolewa katika safari ya kucheza Kombe la Dunia 2014 na pia Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani, mashindano yatakayofanyika nchini Afrika Kusini.
Mchezo wa kuruka kamba hauchukuliwi kwa ushindani mkubwa nchini Tazania.
Wamarekani walifika nchini na kuvutiwa na uchezaji wa Kondo, wakampa mafunzo zaidi kabla ya kumpeleka Marekani na kuwa wafadhili wake pia.
Naibu Mkurugenzi katika Wizara ya Habari, Vijana na Michezo, Juliana Yasoda anasema mchezo huo wa kuruka kamba unakwenda kwa kasi na Wamarekani wameuvalia njuga, ambapo wanaofanya vyema wataingia kwenye mashindano makubwa zaidi.
Yasoda aliwataka Watanzania kuchangamkia michezo mbalimbali kama huo wa kamba, badala ya kukumbatia ile ya mazoea, ambayo kwa bahati mbaya hawafanyi vizuri kimataifa.
Mataifa 14 yalishiriki kwenye mashindano hayo, na zaidi ya wachezaji 100, hivyo sasa Tanzania inapeperusha vyema bendera yake katika mchezo huo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 5565

Trending Articles